Wapo

(B Boy) Eeh
Mmmh mmh
Hivi kwanini nijitutumue
Na dunia sio makazi
Vijineno neno vinisumbue
Hadi nishindwe kazi
Mama alisema mkuku kwa nguruwe
Kuishi na watu kazi
Achambe atukane ata aniue
Nishasamehe mzani ni mzazi

Mwenzenu naficha naficha
Mengi nayoyaona
Kifupi nafunika kombe
Nikiamini kesho nayo siku
Mapicha picha mapicha
Sidhani kama nitapona
Wanangu wa mtaani mniombee
Hii vita ni mchana na usiku
Oooh kuna watu na viatu
Wanatamani milele wawe wao
Ukijituma watasema
Unashinda nao

Oooh ni kama watu kumbe
Ndani wana roho za chatu
Hawatosheki na vikubwa vyao
Wanatamani hata kidogo chako kiwe chao
Mola nipe ujasiri
Kwenye kufanya maamuzi
Zidi nikomaza akili
Isinipoteze miluzi
Uniamshe alfajiri
Kama jana na juzi
Kupata kukosa ni siri
Nawe ndo Mungu baba mwamuzi

Dear Lord, wapo
Iyeiye iye, wapo
Japo ni ngumu kuwaona, wapo
Wapo wasotaka ufanikiwe
Binadamu hawana jeru, wapo
Kila utachofanya watasema, wapo
Wapo wasotaka ubarikiwe
Dear Lord mmh

Watakuita mwanga kibonge
Tena kwa dharau wakucheke
Wanachotaka we uongee
Waseme shukrani ya punda mateke
Kama vipi dem wake tumgongee
Ndiye anayempiga chura teke
Usipoonewa ndonge
Basi ndo ujue hauna makeke
Sikia Konde kwepa bana mjini shule
Ukipata kidogo leta na nao tule
Wachana nao wamesemaga umezoea vya bure
Maana siku zote nyani halioni kundule

Kama baba na mama ndo nguzo ya dunia
Wapende wote
Sio wa kike anacheka wa kiume analialia
Bila msaada wowote

Oooh kuna watu na viatu
Wanatamani milele wawe wao
Ukijituma watasema
Unashinda nao
Oooh ni kama watu kumbe
Ndani wana roho za chatu
Hawatosheki na vikubwa vyao
Wanatamani hata kidogo chako kiwe chao
Mola nipe ujasiri
Kwenye kufanya maamuzi
Zidi nikomaza akili
Isinipoteze miluzi

Uniamshe alfajiri
Kama jana na juzi
Kupata kukosa ni siri
Nawe ndo Mungu baba mwamuzi
Dear Lord, wapo
Iyeiye iye, wapo
Japo ni ngumu kuwaona, wapo
Wapo wasotaka ufanikiwe
Binadamu hawana jeru, wapo
Kila utachofanya watasema, wapo
Wapo wasotaka ubarikiwe
Dear Lord

“Special message to the Youth”
It’s your time now to follow your dreams
No matter what people say stay humble
Stay positive, follow your dream
Believe in God, ease your mind
Ease your mind for Lord
(The Most Wanted Mix)

Chansons les plus populaires [artist_preposition] Harmonize

Autres artistes de Afrobeats