Unanionea

Hivi kweli yupo
Mwenye roho mbaya kukushinda
Maana mi sijaona Duniani
Hivi kweli yupo
Aso na haya kukushinda
Maana mie sijaona sijaona
We mtu gani uko radhi mwenzako ateketee
Wakati unajua dawa yake
Ni kumponya, nihurumie
Ama mtu gani aliefika akaongeza makeke
Na wakati anajua mi kwako ndo napona,
We nihurumie
Mi najua mapenzi
Sio kwichi kwichi tu
Yanayonogaga mazoea Nimekuzoea mmmh

Unanionea, mwenzako siwezi matukio mazito
Unanionea, unanipiga mie
Unanionea, unafanya niamini mapenzi mabaya
Unanionea, lalalaa mmmmh

Na kama kuachana nakubali
Sawa fanya yako
Ila sio lazima unionyeshe uniumize
Au kisa unajua
Unaniacha bado nakuhitaji
Ndo unaona bora unikomeshe Unilize eeeh
Ah poa poa,
Nishajua vya utamu Vinakuwaga vya uchungu
Ili doa doa milima haikutani
Japo najua mapenzi
Sio kwichi kwichi tu
Yanayonogaga mazoea
Nimekuzoea mmmh

Unanionea, mwenzako siwezi matukio mazito
Unanionea, unanipiga mie
Unanionea, unafanya niamini mapenzi mabaya
Unanionea, lalalaa
Unanionea, unanionea bure
Hata Bonga anajua unanionea
Chino anajua, unanionea

Chansons les plus populaires [artist_preposition] Marioo

Autres artistes de